Laetoli ni eneo karibu na Bonde la Oltupai (Tanzania), km 45 kusini kwake, ambapo mwaka 1972 Mary Leakey aligundua nyayo za kale (miaka milioni 3.7 iliyopita) za zamadamu watatu waliotembea kwa miguu miwili.
Mwaka 2015 ushirikiano wa watafiti wa Tanzania na wa Italia uliwezesha kugundua nyayo nyingine mbili za msafara huohuo, za mmojawapo zikiwa ndefu sana kuliko nyingine.