Lamu | |
Mahali pa mji wa Lamu katika Kenya |
|
Majiranukta: 2°16′0″S 40°55′0″E / 2.26667°S 40.91667°E | |
Nchi | Kenya |
---|---|
Kaunti | Lamu |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 25,385 |
Lamu ni mji mkubwa wa kisiwa cha Lamu kwenye pwani ya Kenya wenye wakazi 25,385 (2019[1]). Mji huo ni pia makao makuu ya Kaunti ya Lamu.
Mji upo upande wa kaskazini-mashariki wa kisiwa kando ya mfereji unaotenganisha visiwa vya Lamu na Manda. Mfereji huo ni bandari asilia inayohifadhiwa dhidi ya dhoruba na mawimbi makali ya bahari.