Maajabu ya dunia ni orodha ya majengo saba ya pekee iliyojulikana na Wagiriki wa Kale. Wagiriki waliita majengo hayo ΤÀ ΕΠΤÀ ΘΕÁΜΑΤΑ ΤΗΣ ΟΙΚΟΥΜÉΝΗΣ (ΓΗΣ) ta hepta theamata tes oikumenes (ges) - Maajabu saba ya dunia inayokaliwa).
Mara ya kwanza majengo ya ajabu yaliorodheshwa na mwandishi Herodoti mnamo 450 KK. Ilhali maandiko yake hayakuhifadhiwa, habari hii inatokana na waandishi wengine waliomrejea. Kulikuwa na orodha tofauti[1][2] lakini ile inayojulikana na kutajwa zaidi ni ile ya Antipater wa Sidon[3]
Ilhali orodha hii ilikusanywa na waandishi wa Ugiriki ya Kale kuna majengo tu yaliyojulikana katika ustaarabu huo. Kwa hiyo hakuna mifano kutoka Uhindi, China, Asia ya Mashariki, Amerika, Afrika kusini ya Sahara wala Ulaya ya Kaskazini.
Majengo ya orodha ya Antipater hayakudumu hadi leo, isipokuwa Piramidi za Giza. Mengine yaliharibika kutokana na matetemeko ya ardhi au kubomolewa, tena hadi leo hapajulikani mahali pa "Mabustani ya Semiramis". Sanamu na picha za kuchongwa kutoka Kaburi la Mausolo na Hekalu la Artemis zilikusanwa na kuhifadhiwa katika Makumbusho ya Britania mjini London, Uingereza.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)