Maandamano (kutoka kitenzi "andaa" kilichonyambuliwa kwa viambishi -ma- na -na-; kwa Kiingereza procession, kutoka Kilatini processio, pia cortege) ni kundi la watu wanaotembea pamoja kwa utaratibu maalumu.
Yametumika nyakati zote na mahali pote kwa ajili ya ibada, siasa n.k. inavyoonekana k.mf. katika michoro mingi ya zamani, hasa ya mazishi na ya kushangilia ushindi vitani.