Mafua ya kawaida | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Kundi Maalumu | Family medicine, infectious diseases, otolaryngology |
ICD-10 | J00.{{{3}}} |
ICD-9 | 460 |
DiseasesDB | 31088 |
MedlinePlus | 000678 |
eMedicine | med/2339 |
MeSH | D003139 |
Mafua ya kawaida (pia mafua ya kuku au mafua tu; kwa Kiingereza: common cold, nasopharyngitis, rhinopharyngitis), ni ugonjwa wa kuambukizwa unaoathiri sehemu ya juu ya mfumo wa upumuaji, hasa pua na shingo.
Dalili ni pamoja na kikohozi, utoaji kamasi puani (rhinorrhea), na homa. Dalili kwa kawaida hupotea baada ya siku saba hadi kumi, ingawa baadhi ya dalili zake zinaweza zikakaa hadi wiki tatu.
Mafua ya kawaida husababishwa na virusi mbalimbali; zaidi ya mia mbili zinajulikana kusababisha mafua ya kawaida. Virusi vya jamii ya rinovirusi (rhinovirus) ndivyo visababishi vikuu.
Maambukizo makali ya pua, mianzi ya pua, koo au zoloto (maambukizi ya sehemu ya juu ya njia ya hewa: URI au URTI) yanabainishwa na eneo la mwili ambalo limeathirika zaidi. Mafua ya kawaida yanaathiri pua, yanavimbisha kolomeo, koo, na yanavimbisha mianzi ya pua. Dalili zinatokana na mfumo wa kinga unaopambana na maambukizi, si kwa sababu ya uharibifu wa seli mwilini unaoletwa na virusi. Kuosha mikono ni njia ya msingi ya kuzuia maambukizi. Kuna ushahidi unaounga mkono uvaaji kitambaa usoni ni bora zaidi.
Hakuna tiba ya mafua ya kawaida, lakini dalili zinaweza kutibiwa. Ni ugonjwa unaoambukiza sana binadamu. Kwa kawaida watu wazima wanaambukizwa mara mbili au tatu kwa mwaka. Kwa kawaida watoto huwa wanapata mafua mara sita au mara kumi na mbili kwa mwaka. Ugonjwa huo umekuwa ukiambukiza binadamu tangu zamani.