Majira ya baridi (pia: kipupwe; kwa Kiingereza Winter) ni mojawapo kati ya majira manne ya kanda za wastani, na halijoto yake ni ya baridi kuliko majira mengine. Ni kinyume cha majira ya joto au chaka.
Pengine baridi inakuwa kali sana na kuendana na barafuto: ndiyo maana maeneo mengine ya dunia hayana wakazi wa kudumu, hasa bara la Antaktiki.
Yanafuata majira ya kupuputika majani (kwa Kiingereza Fall au Autumn) na kutangulia majira ya kuchipua (kwa Kiingereza Spring).
Majira hayo yanatokea duniani kwa nyakati tofauti kadiri eneo husika lilivyo kaskazini au kusini kwa ikweta. Hata katika nchi ileile, kwa mfano Kenya, majira ni tofauti upande huu na upande huu wa ikweta.
Majira hayo tofauti hupatikana zaidi katika ukanda wa tropiki.