Matabeleland Kaskazini

Mkoa wa MAtabeleland Kaskazini katika Zimbabwe
Mkoa wa MAtabeleland Kaskazini katika Zimbabwe

Matabeleland Kaskazini ni mkoa wa Zimbabwe upande wa kaskazini wa Bulawayo. Mkoa umepakana na Bulawayo, Matabeleland Kusini, Midlands na Mashonaland Magharibi. Kuna mipaka ya kimataifa na Zambia upande wa kaskazini kwenye mto Zambezi na Botswana upande wa kusini-magharibi.

Kuna wakazi 828,000 (2022[1]) katika eneo la kilomita za mraba 75,025.

Makao makuu ya mkoa yapo mjini Lupane.

Miji mikubwa kidogo ni Hwangwe na Victoria Falls.

Mkoa unavutia watalii hasa kwa maporomoko ya Victoria Falls na hifadhi ya taifa ya Hwangwe.

  1. https://www.citypopulation.de/en/zimbabwe/cities/

Matabeleland Kaskazini

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne