Mboji

Jalala la pamoja Ujerumani.

Mboji (pia: "matanda"; kwa Kiingereza humus, compost) ni mata ogania katika udongo. Inafanywa na vipande visivyo na uhai tena vya mimea na wanyama. Inatokea katika mchakato wa kuoza kwa mimea na pia wanyama. Ni sehemu muhimu ya udongo maana inaongeza rutuba yake. Tofauti na mchanga mtupu inaweza kushika maji kama sifongo. Pia ina virutubishi vingi ndani yake pamoja na nitrojeni.

Mwanzoni mboji bado huwa na mabaki yanayoonekana kama vipande vya majani au matawi. Kadiri vinavyoendelea kuoza vinavunjwa na wanyama wadogo wanaoishi humo kama sisimizi, minyoo, wadudu wa aina nyingi pamoja na bakteria na fungi, halafu havionekani tena vile na inayobaki ni mata nyeusi-nyeusi.

Udongo wenye rutuba huwa na takaba la juu ya sentimita kadhaa penye kiasi cha mboji.

Wakulima mara nyingi wanajitahidi kuongeza kiasi cha mboji maana ni mbolea ogania tena bora kuliko mbolea ya kikemia. Wenye bustani mara nyingi hukusanya majani na kuyaweka mahali pa kuoza wakiangalia mazingira inayowezesha oksijeni kufika ndani yake kwa kuwa inawasaidia wanyama wadogo kufanya kazi ya kuvunja mata ogania.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mboji kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Mboji

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne