Mjusi

Mjusi
Mjusi madoa-macho (Chalcides ocellatus)
Mjusi madoa-macho (Chalcides ocellatus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli ya juu: Tetrapoda
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Lacertilia (Pia Sauria)
Ngazi za chini

Kladi zinazokubaliwa:

Mijusi ni wanyama watambaachi katika oda Squamata ya ngeli Reptilia. Spishi nyingi sana zina miguu minne, lakini kuna spishi nyingine zilizopoteza miguu miwili au miguu yote. Urefu wa mijusi unaanzia kutoka sm kadhaa (spishi ndogo za kinyonga na mjusi-kafiri) hadi m 3 (joka wa Komodo).

Mijusi hula nyama, spishi ndogo hula wadudu na spishi kubwa hula vertebrata pia mpaka joka wa Komodo anayekula wanyama hadi ukubwa wa nyati-maji. Hata hivyo spishi nyingi hula mimea na/au matunda pia.


Mjusi

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne