Mkoa wa Ruvuma |
|
Mahali pa Mkoa wa Ruvuma katika Tanzania | |
Majiranukta: 11°0′S 36°0′E / 11.000°S 36.000°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Wilaya | 8 |
Mji mkuu | Songea |
Serikali | |
- Mkuu wa Mkoa | Christine G. Ishengoma |
Eneo | |
- Jumla | 63,498 km² |
Idadi ya wakazi (2022) | |
- Wakazi kwa ujumla | 1,848,794 |
Tovuti: http://www.ruvuma.go.tz/ |
Mkoa wa Ruvuma ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania.
Umepewa jina kutokana na mto Ruvuma ambao ni mpaka wake wa kusini na Msumbiji. Umepakana na Ziwa Nyasa na Mkoa wa Morogoro upande wa magharibi, mikoa ya Iringa na Lindi upande wa kaskazini na Mkoa wa Mtwara upande wa mashariki.
Makao makuu ya mkoa yako Songea mjini.