Mkoa wa Shinyanga ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye msimbo wa posta 37000. Mkoa umepakana upande wa kaskazini na mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera, upande wa kusini na Mkoa wa Tabora. Mkoa wa Kigoma uko upande wa magharibi, na mkoa wa Simiyu upande wa mashariki.
Makao makuu yako mjini Shinyanga.