Mkoa wa Unguja Kaskazini ni mmojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye Postikodi namba 73000. Uko Unguja ambayo ni kisiwa kikubwa cha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
Makao makuu ya mkoa yako Mkokotoni.
Kuna wilaya mbili ambazo ni Kaskazini Unguja 'A' (105,780 mwaka 2012 na 157,369 mwaka 2022) na Kaskazini Unguja 'B' (81,675 mwaka 2012 na 99,921 mwaka 2022)[1][2].
Eneo la mkoa ni km² 470 ambako kuna jumla ya wakazi 257,290 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022[3].
Wengi wanajishughulisha na uvuvi na kilimo. Sehemu ya mashariki ya mkoa kuna kilimo cha karafuu.
Upande wa magharibi utalii umeanza kuwa muhimu. Eneo la Ras Nungwi ni sehemu moja yenye mahoteli ya watalii wa nje.
Kisiwa cha Tumbatu ni sehemu ya mkoa huu.
Miji ya mkoa ndiyo Mkokotoni, Mahonda na Gamba.