Mlangobahari wa Otranto

Ramani inayoonyesha eneo la Mlangobahari wa Otranto.

Mlangobahari wa Otranto (kwa Kiingereza: Strait ya Otranto) unaunganisha Adria na Bahari ya Ionia. Unatenganisha Italia na Albania. Upana wake karibu na Salento ni chini ya kilomita 72. [1] Jina linatokana na mji wa Italia wa Otranto.

Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, mlango huo ulikuwa na umuhimu wa kimkakati. Wanamaji wa ushirikiano wa Italia, Ufaransa, na Uingereza walizuia manowari za Austria-Hungaria kutoka kwenye Adria na kuingia Bahari ya Mediteranea .

  1. Cushman-Roisin, Benoit; Gacic, Miroslav; Poulain, Pierre-Marie; Artegiani, Antonio (2001). Physical Oceanography of the Adriatic Sea: Past, Present and Future. Springer Netherlands. uk. 93. ISBN 978-1-4020-0225-0.

Mlangobahari wa Otranto

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne