Mnara wa Babeli ni jengo kubwa linalotajwa katika Biblia kwenye Kitabu cha Mwanzo 11:1-9. Kufuatana na taarifa hii mnara ulijengwa pamoja na mji wa Babeli kama kilele chake.
Katika mapokeo ya Mwanzo 11 Babeli ulikuwa mji wa kwanza uliojengwa baada ya gharika kuu. Binadamu waliamua kuwa na jengo kubwa katika mji na kilele chake kifike mbinguni. Mpango huu haukumpendeza Mungu aliyechanganya lugha ya watu ambao hivyo walilazimika kuachana baadaye bila ya kukamilisha mnara wao.
Kihistoria si wazi ni kipindi gani kinachoangaliwa katika simulizi la Mwanzo 11. Inaonekana ya kwamba wasimulizi walikuwa na habari za piramidi au zigurati kubwa zilizokuwepo Babeli na penginepo katika Mesopotamia.