Mongolia ya Kichina huitwa pia "Mongolia ya Ndani" ni eneo la kujitawala ndani ya Jamhuri ya Watu wa China iliyokuwa eneo la makabila ya Wamongolia ingawa siku hizi Wahan ni wakazi wengi. Wamongolia wenyewe mara nyingi huita eneo "Mongolia ya Kusini".
Imepakana na Jamhuri ya Mongolia, Urusi na majimbo mbalimbali ya China. Eneo lake ni milioni 1.18 km² (takriban 12% za China) linalokaliwa na watu milioni 24 (2004). Mji mkuu ni Hohhot.
Lugha rasmi ni Kichina cha Mandarin na Kimongolia.