Mpira wa kikapu ni aina ya michezo inayopendwa katika sehemu nyingi za dunia na watu wengi hutamani mchezo huu.
Mara nyingi hufanywa ukumbini wakati timu mbili za wachezaji wanajaribu kuingiza mpira katika kikapu cha timu nyingine.
Vikapu viko mwishoni mwa upande mwembamba wa uwanja kwa urefu wa mita 3.05.
Kila timu huwa na wachezaji 5 uwanjani na hadi wachezaji wa kando 7 walio tayari kuchukua nafasi ya mchezaji mwingine muda wowote.
Kila goli katika kikapu cha upande mwingine linahesabiwa kama pointi 2 au 3, kutegemeana na umbali wa kurusha. Goli la penati huleta pointi 1 tu.