Msikiti

Masjid al-Haram huko Maka, Saudia, ndio msikiti muhimu zadi katika Uislamu.

Msikiti ni mahali pa ibada kwa waumini wa dini ya Uislamu, ambapo lengo kuu ni kutekeleza wajibu wa sala chini ya imamu. Hata hivyo ukumbi unaweza kutumika pia kwa kuelimishana na kujadiliana, kama ilivyokuwa kwa masinagogi ya Wayahudi.

Waislamu wengi mara nyingi huita msikiti kwa kutumia jina la Kiarabu, ambalo ni masjid - مسجد — inatamkwa [ˈmæsʤɪd] (wingi wake ni: masajid kwa Kiarabu: مساجد — inatamkwa /mæˈsæːʤɪd/).

Kutoka Uarabuni misikiti imeenea duniani kote, ikiunganishwa mara nyingine na minara.

Baadhi yake inatumia sanaa ya hali ya juu.


Msikiti

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne