Msitu ni mkusanyiko wa uoto asilia unaojumuisha miti mingi ya aina mbalimbali (kwa mfano: mipingo, mikoko n.k.) mimea na nyasi ambazo huweza kuwa fupi au ndefu.
Misitu inaweza kuwa za aina mbili:
Misitu ya asili ni misitu ambayo huota yenyewe bila kupandwa na mwanadamu. Kwa mfano, msitu wa Udzungwa (Mkoa wa Morogoro, Tanzania) ni kivutio kikubwa cha watalii, hivyo kupitia msitu huu nchi inajipatia fedha za kigeni.
Misitu isiyo ya asili ni misitu ambayo hupandwa na mwanadamu kwa malengo mbalimbali.
Ndiyo tofauti kati ya misitu ya asili na isiyo ya asili.