Mitume wa Yesu |
---|
|
Mtume Yohane (aliishi karne ya 1 B.K.) alikuwa mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu, ambaye alipendwa na mwalimu wao kuliko wenzake wote.
Pamoja na kaka yake Yakobo na rafiki yao Petro alishuhudia tukio la Yesu Kugeuka sura na la kuteseka katika bustani ya Getsemane, akapokea kutoka kwake Bikira Maria kama mama akiwa chini ya msalaba.
Mapokeo ya Ukristo yanamuona kuwa mwandishi wa Injili ya Yohane, wa barua tatu (Waraka wa kwanza wa Yohane, Waraka wa pili wa Yohane, Waraka wa tatu wa Yohane) na wa Kitabu cha Ufunuo.
Katika maandishi hayo anajitokeza mwanateolojia ambaye, kisha kujaliwa kutazama utukufu wa Neno aliyefanyika mwili, alitangaza aliyoyaona kwa macho yake [1].