Mugumu | |
Mahali pa Mugumu katika Tanzania |
|
Majiranukta: 1°50′21″S 34°40′28″E / 1.83917°S 34.67444°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Mara |
Wilaya | Serengeti |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 13,288 |
Mugumu ni mji mdogo na makao makuu ya Wilaya ya Serengeti katika Mkoa wa Mara, Tanzania, yenye postikodi namba 31601.
Ni nyumbani kwa hifadhi maarufu Duniani Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 13,288 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ya Mugumu ilikuwa na wakazi wapatao 10,226 waishio humo. [2]
Wakazi wengi wa Mugumu ni Wakurya; pia kuna makabila mengine kama vile Waikoma, Wanata, Waisenye, Wakisii na wengine wengi wanaofanya mji huo kuwa na mchanganyiko wa makabila.
Zaidi ya asilimia 50 ya wakazi wa hapo ni waumini wa dini ya Kikristo.