Nairobi | |||
| |||
Mji wa Nairobi (Kenya) |
|||
Majiranukta: 1°17′S 36°49′E / 1.283°S 36.817°E | |||
Nchi | Kenya | ||
---|---|---|---|
Kaunti | Nairobi | ||
Idadi ya wakazi (2019) | |||
- Wakazi kwa ujumla | 4,397,073 | ||
Tovuti: nairobi.go.ke |
Nairobi ni mji mkuu wa jamhuri ya Kenya na vilevile mojawapo ya kaunti za Kenya.
Kulingana na sensa ya mwaka 2019, Nairobi ina wakaaji 4,397,073 katika eneo la km2 696 (sq mi 269).
Pamoja na vitongoji vyake, Nairobi ni mji wa 12 kwa ukubwa barani Afrika.
Jina Nairobi limetokana na neno la Kimaasai, Enkarenairobi, linalomaanisha "mahali penye maji baridi."
Lugha zote za Kenya huzungumzwa Nairobi, lakini hasa ni Kiingereza na Kiswahili pamoja na Sheng.