Nembo ni alama au mchoro unaowakilisha au unaosimama badala ya mtu, wazo, picha inayoonekana au kitu fulani. Nembo zinachukua mfumo wa maneno, sauti, mawazo au picha inayoonekana ambazo zinatumika kuelezea mawazo au imani nyingine.
Kwa mfano, oktagoni nyekundu inaweza kuwa nembo inayowakilisha "SIMAMA". Katika ramani mstari wa rangi ya buluu unaweza kuwakilisha mto. Tarakimu ni nembo ya namba. Herufi za alfabeti zinaweza zikawa nembo za sauti. Majina binafsi ni nembo zinazowakilisha watu. Waridi jekundu linaweza kuwakilisha upendo.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |