Ngeli ni makundi ya kisarufi ya majina katika lugha ya Kiswahili na lugha nyingine za Kibantu.
Kwa maneno mengine, ngeli za nomino ni utaratibu unaotumika kuweka nomino katika matabaka au makundi yanayofanana.
Katika mifano hiyo juu tunaona kwamba sentensi a, b na c ziko sahihi wakati sentensi d si sahihi, kwa sababu imekiuka upatanisho wa kisarufi. Kwa maana hiyo sentensi ‘a’ ipo katika ngeli ya YA-YA na sentensi b na c zipo katika ngeli ya LI-YA. Sentensi si sahihi kwa sababu nomino maji haina umoja, kwa hiyo haiwezi kuingia katika ngeli ya LI-YA. Kwa msingi huo ngeli za nomino huzingatia sana upatanisho wa kisarufi.
Kwa ujumla, ngeli za Kiswahili huainishwa kulingana na viambishi mbalimbali ambavyo nomino tofauti huchukua katika umoja na wingi.