Njaa ni hali ya kukosa chakula kinachohitajiwa na mwili ili kujimudu.
Sababu zake zinaweza kuwa mbalimbali, kama vile vita, ukame, maradhi ya mimea, wadudu waharibifu, utovu wa ustadi katika uzalishaji na utunzaji wa mazao, ugumu wa mawasiliano n.k.
Kila bara liliwahi kupatwa na hali hiyo katika historia, na bado hiyo ni tishio kwa nchi mbalimbali, pia kutokana na sababu mpya, kama vile utandawazi, matumizi ya mazao kwa ajili ya kuendesha mashine kiekolojia.