Nonini (jina lake haswa ni Hubert Nakitare, amezaliwa 1 Oktoba 1982) ni msanii wa nyimbo aina ya hip hop kutoka nchini Kenya; awali akisajiliwa na "Calif Records", lakini baadaye alijiunga na "Homeboyz Productions".
Yeye alijitosa kwenye ulingo wa muziki wa mijini nchini Kenya kupitia wimbo wake "Nonini ni Nani?" kupanda kwa umaarufu wake kitaifa na kikanda hakuanza hata hivyo mpaka alipotoa wimbo wake "Manzi wa Nairobi" mwaka 2002, wimbo ambao ulisifu uzuri wa wanawake wa Kenya na kufuatiliwa na wimbo "Weh Kamu". Yeye aliendelia kwa kutoa albamu yake "Hanyaring Game" mwishoni mwa mwaka wa 2004 ambayo ilihusisha wimbo maarufu "Keroro" neno la kisheng lenye maana ya pombe ya bia. Nonini anajulikana kwa kutoa wimbo wa kwanza wa Genge mapema katika kazi yake ya uimbaji.
Baadaye, wimbo Nani mwenza, kwa ushirikiano na mwanamuziki kutoka Tanzania Juma Nature, uliweza kujulikana kikanda. Katika ubunifu mkubwa hivi karibuni, ameshirikiana pamoja na msanii "Nameless" kuunda wimbo wa kitaifa wa Ijumaa ujulikanao kama "furahi day" ambao umechezwa sana katika vituo vya utangazaji. Nyimbo zote mbili ziko kwenye albamu yake ya pili Mwisho Ya Mawazo,iliyotolewa mwaka 2007. Albamu yake iliwahusisha wanamuziki wakiwemo Nyota Ndogo, Mercy Myra, Profesa Jay na Q-Chief Agosti 2007, Nonini alikuwa miongoni mwa Wakenya 100 wenye ushawishi mkubwa kama ilivyochanguliwa na gazeti la "The Standard" Nonini alishinda tuzo bora la kimuziki la Chaguo La Teeniez mwaka 2008 kwa video yake ya "Mtoto Mzuri" katika Mwaka wa 2009 alitajwa kama Balozi wa "International Lifestyle" na Chuo Kikuu cha Limkokwing nchini Malaysia.
Nonini ni nusu Mluhya na nusu Mkamba.