Nyuzi (pia: digrii kutoka neno la Kiingereza) ni kizio cha kupimia pembe . Msingi wake ni mzunguko kamili wa duara unaogawiwa kwa sehemu 360°. Kwa kawaida nyuzi moja huandikwa kama 1°.
Nusuduara ina 180°. Pembemraba ina 90°. Jumla ya pembe ndani ya pembetatu ni 180°, ndani ya mstatili ni 360°.
Nyuzi inaweza kugawiwa tena kwa dakika ya tao na sekunde ya tao. Dakika ya tao ni sehemu ya 60 na sekunde ya tao ni sehemu ya 3600 ya nyuzi moja.