Makala haina vyanzo vya kutosha
Makala (au sehemu ifuatayo ya makala) inatoa habari bila kuonyesha vyanzo au uthibitisho wowote.
|
Paka | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Paka miguu-myeusi
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Jenasi 10: |
Paka ni wanyama mbuai wa nusufamilia Felinae katika familia Felidae. Spishi nyingine zinaitwa duma, simbamangu na mondo. Nyingi ni ndogo kama paka-kaya lakini spishi kama duma, linksi na puma ni kubwa zaidi sana. Isipokuwa simbamangu, Asian golden cat, puma na pengine paka-msitu, paka wote wana milia na/au madoa. Paka hukamata mawindo aina yo yote lakini ukubwa wa mawindo unafuatana na ukubwa wa spishi ya paka. Spishi nyingine zinatokea msitu na nyingine zinatokea maeneo wazi.