Papa Adrian VI (2 Machi 1459 – 14 Septemba 1523) alikuwa Papa kuanzia tarehe 9 Januari/31 Agosti 1522 hadi kifo chake[1]. Alitokea Utrecht, Uholanzi[2]. Alikuwa Mholanzi pekee kuwa Papa, na alikuwa Papa wa mwisho asiye Mwitalia hadi Papa Yohane Paulo II kutoka Polandi alipochaguliwa miaka 455 baadaye [3].
Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Adriaan Florensz, hivyo hakubadili jina la ubatizo alipochaguliwa kuwa Papa, tofauti na watangulizi na waandamizi karibu wote wa milenia ya pili.
Alimfuata Papa Leo X akafuatwa na Papa Klementi VII.