Papa Leo X (11 Desemba 1475 – 1 Desemba 1521) alikuwa Papa kuanzia tarehe 11/19 Machi 1513 hadi kifo chake[1]. Alitokea Firenze, Italia[2].
Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Giovanni di Lorenzo de' Medici.
Alimfuata Papa Julius II akafuatwa na Papa Adrian VI.
Leo X ndiye aliyemtenga Martin Luther na Kanisa Katoliki tarehe 3 Januari 1521.