Pierre Curie (15 Mei 1859 Paris/Ufaransa - 19 Aprili 1906) alikuwa mwanafizikia Mfaransa aliyepokea Tuzo ya Nobel ya Fizikia kwa mwaka 1903 pamoja na mke wake Marie Curie na Henri Becquerel.
Pamoja na mke wake alichunguza misingi ya sumakuumeme. Maelezo yao yaliunda misingi wa kuelewa unururifu wa kinyuklia.
Pierre Curie alishirikiana na mkewe Marie Curie pia katika ugunduzi wa elementi za poloni na radi hata baada ya kifo chake, mke akapata tuzo ya Nobel ya kemia.
Pierre Curie alikufa kutokana na ajali ya gari.