Plau (kut. Kiing. plough (UK) au plow (US)) ni mashine sahili ya kulimia ardhi kwenye kilimo.
Plau huvutwa shambani kwa nguvu ya trekta au mashine, mnyama au pia ya kibinadamu. Ulimi wa plau unakata ardhi na kuigeuza. Kwa njia hii ardhi inalainishwa na tabaka za chini zenye lishe mpya ya mimea zinapelekwa juu. Vilevile majani yasiyotakiwa yanachimbwa chini ya ardhi hivyo kuipa nafasi mimea mipya kutokana na mbegu unaopandwa.