Kwa ngurumo ya umeme tazama radi
Radi | |
---|---|
Jina la Elementi | Radi |
Alama | Ra |
Namba atomia | 88 |
Uzani atomia | 226,0254 u |
Valensi | 2, 8, 18, 32, 18, 8, 2 |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | 973 K (700 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 2010 K (1737 °C) |
Radi (kutoka Kilatini "radius") ni elementi katika mfumo radidia yenye alama Ra.
Namba atomia ni 88 na uzani atomia ni 226.0254.
Jina limechaguliwa kutokana na tabia yake ya ununurifu: kwa Kilatini "radius" yamaanisha "mwale" au "mwonzi".
Kikemia radi ni metali ya udongo alikalini yenye rangi nyeupe. Lakini inaoksidisha haraka kushika rangi nyeusi.
Radi ni haba sana hutokea kama sehemu ya mchanganyiko wa madini kadhaa pamoja na urani. Hutokea hasa kama isotopi ya 226Ra yenye nusumaisha ya miaka 1,602 ikibadilika kuwa gesi ya radoni.