Robert Mangaliso Sobukwe

Robert Mangaliso Sobukwe (1924-1978) alikuwa mwanasheria na mwanasiasa wa Afrika Kusini aliyeanzisha Pan Africanist Congress kupinga ubaguzi wa rangi nchini. Kwa ajili hiyo alifungwa kwa muda mrefu. Alikuwa muasisi wa chama hicho kilichopigania uhuru wa Waafrika kikijitenga kutoka kwa African National Congress, pia anahusishwa na kuandaa maandamano ya kihistoria ya Shapeville mnamo 1960 yaliyopinga sheria ya Weusi kutembea na vitambulisho ambapo mamia ya watu waliuawa na kujeruhiwa kisha Sobukwe kuswekwa jela kunako visiwa vya Rubeni kwa miaka tisa.

Sobukwe alifariki mwaka 1978 kwa saratani na mapafu licha ya wengine kudai kuwa alipewa sumu akiwa jela.


Robert Mangaliso Sobukwe

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne