Samia Suluhu Hassan | |
Rais
| |
Aliingia ofisini 17 Machi 2021 | |
tarehe ya kuzaliwa | 27 Januari 1960 Usultani wa Zanzibar |
---|---|
utaifa | Mtanzania |
chama | Chama Cha Mapinduzi |
ndoa | Hafidh Ameir |
watoto | Mwanu Hafidh Ameir,Wanu Hafidh Ameir |
mhitimu wa | Chuo Kikuu cha Mzumbe Chuo Kikuu cha Manchester Chuo Kikuu Huria cha Tanzania SNHU |
dini | Uislamu |
Samia Suluhu Hassan (alizaliwa 27 Januari 1960) ni Rais wa 6 wa Tanzania na mwanachama wa chama tawala cha Chama Cha Mapinduzi.[1]
Kabla ya kuwa rais kutokana na kifo cha John Magufuli, kilichotokea tarehe 17 Machi 2021, Suluhu alikuwa makamu wa rais kwa sababu ya kuwa mgombea mwenza katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.[2]
Tarehe 5 Novemba 2015 aliapishwa kama makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa mwanamke wa kwanza kufikia cheo hicho, akarudia baada ya uchaguzi mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2020.
Sasa amekuwa rais wa kwanza mwanamke na rais wa Pili kutoka Zanzibar Wa kwanza Akiwa ni Ally Hassan Mwinyi Rais wa awamu ya Pili.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)