Shirika la Yesu (kwa Kilatini Societas Iesu, kifupi S.J. au S.I. au SJ au SI) ni shirika kubwa la watawa wanaume 15,842 (2018) katika Kanisa Katoliki, lililoenea katika nchi 112 za kontinenti 6.
Wanashirika wanaitwa Wayesuiti au Wajesuiti na ni maarufu pia kwa elimu yao ya juu katika fani mbalimbali, za kidunia na za kidini.