Shujaa (kutoka neno la Kiarabu; kwa Kiingereza: hero au heroine, kutoka Kigiriki: ἥρως, hḗrōs, yaani "mlinzi" au "mtetezi"[1]) ni mtu ambaye ameshinda juu ya jambo fulani, kwa mfano vita, au anaweza kukabili jambo lolote kwa ujasiri, bila kuzuiwa na woga.
Katika fasihi ni mhusika mkuu wa utendi.[2]
Mifano ya mashujaa ni kuanzia wahusika wa kubuniwa wa kale kama Gilgamesh, Akile na Ifigenia, hadi watu halisi wa kale kama Yoana wa Arc au Sophie Scholl, mashujaa wa siku hizi kama Alvin York, Audie Murphy na Chuck Yeager, tena mashujaa wa katuni kama Superman, Spider-Man, Batman na Captain America.