Shukrani (pia: shukurani; kutoka neno la Kiarabu) ni tendo la kukubali zawadi, hisani au fadhili yoyote kutoka kwa mwingine.
Moyo wa shukrani ni sifa mojawapo muhimu katika mafungamano ya watu na imezingatiwa na fasihi na dini mbalimbali hata upande wa Mungu[1]. Wanaofuata dini wanaelekea kuwa na shukrani zaidi katika maisha yao yote[2][3].
Kinyume chake utovu wa shukrani ni jambo linalovuruga sana mahusiano katika jamii, kuanzia ndani ya familia, na imezingatiwa na elimunafsia katika kuchunguza chanzo chake, kwa kuwa inamzuia mtu kufaidika na moyo huo [4].