Simu

Simu ya mezani
Simu ya mikononi
Simujanja

Simu (kutoka Kiarabu سیم, sim, inayomaanisha "waya") ni kifaa cha elektroniki kinachotumika kwa mawasiliano ya mbali kwa kutumia sauti, ujumbe wa maandishi, au njia nyingine za kidigitali.

Ina uwezo wa kupokea na kutuma taarifa sehemu mbalimbali kupitia mtandao wa mawasiliano, kama vile simu za mkononi au simu za mezani. Simu pia inaweza kuwa na huduma nyingine kama kamera, kumbukumbu, na uwezo wa kupata mtandao wa intaneti, na hutumika kwa madhumuni mengi kama vile mawasiliano ya binafsi, kazi, au burudani.

Awali simu ilihitaji iunganishwe na nyaya, lakini leo hii inaweza kutumia redio. Hiyo inaitwa nyayatupu, siwaya au simu bila waya.


Simu

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne