Skandinavia ni eneo la Ulaya ya Kaskazini. Kwa kawaida neno linataja nchi tano za Norwei, Uswidi, Udani, Ufini na Iceland.
Kwa maana nyingine "Skandinavia" ni nchi mbili za rasi ya Skandinavia pekee, yaani Norwei na Uswidi.
Lugha za Skandinavia ziko karibu sana; zote ni Kigermanik ya Kaskazini isipokuwa Kifini ambacho ni lugha yenye asili ya Asia.