Soko la hisa (kwa Kiingereza "stock exchange") ni mahali pa biashara ya hisa za makampuni.
Mara nyingi "soko la hisa" lamaanisha taasisi au jengo ambako biashara hii inafanywa. Lakini jina hili laweza pia kumaanisha jumla ya biashara ya hisa katika nchi fulani au katika tawi la uchumi (ing. "share / stock market") kwa kujumlisha taasisi mbalimbali katika nchi au biashara kwa njia ya intaneti.