Swala

Kwa swala kama ibada ya Kiislamu, taz. Swalah.
Swala
Swala tomi (Eudorcas thomsonii)
Swala tomi
(Eudorcas thomsonii)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyana wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Artiodactyla (Wanyama wenye vidole viwili au vinne mguuni)
Nusuoda: Ruminantia (Wanyama wanaocheua)
Familia: Bovidae (Wanyama walio na mnasaba na ng'ombe)
J. E. Gray, 1821
Ngazi za chini

Nusufamilia 3, jenasi 12:

Swala ni wanyama walao nyasi katika nusufamilia Antilopinae, Aepycerotinae na Pantholopinae za familia Bovidae. Hupatikana katika maeneo yenye nyasi fupi fupi na vichaka vifupi fupi hasa kwenye maeneo mengi ya hifadhi katika Afrika. Spishi nyingine hukimbia kilometa 80 kwa saa na zina uwezo wa kuruka mita 7 hadi 8 juu akiwa kwenye kasi. Rangi yao ni ya mchanga na nyeupe kidogo kwenye koromeo na sehemu ya chini ya mkia. Maadui yao wakubwa ni simba, chatu na chui.


Swala

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne