Tamathali za semi ni maneno, nahau au sentensi ambazo hutumiwa na wasanii ili kutia nguvu katika maana, mitindo na hata sauti katika maandishi ama kusema. Wakati mwingine hutumiwa kama njia ya kuipamba kazi ya fasihi na kuongeza utamu wa lugha [1]. Hii ina maana kwamba ili msomaji wa kazi yoyote ya fasihi apate ujumbe hana budi kufikiri kwa kina.
Tamathali hizo ni kama vile: balagaha, ritifaa, sitiari, tabaini, tanakalisauti, tashbiha, tashihisi, tashtiti, tasifida.