Titani | |
---|---|
Jina la Elementi | Titani |
Alama | Ti |
Namba atomia | 22 |
Mfululizo safu | Metali |
Uzani atomia | 47.867 |
Valensi | 2, 8, 10, 2 |
Ugumu (Mohs) | 6.0 |
Kiwango cha kuyeyuka | 1941 K (1668 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 3560 K (3287 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 0.41 % |
Hali maada | mango |
Titani ni elementi na metali yenye namba atomia 22 na alama Ti katika mfumo radidia wa elementi. Ni elementi mpito inayotafutwa sana kwa sababu ni nyepesi na imara sana na haiathiriwi rahisi kikemia, yaani haishikwi na kutu.
Kwa hiyo inatumiwa kama sehemu za aloi za chumapua mbalimbali kwa mfano kwa eropleni au mashine zinazokusudiwa kwa kazi kwenye maji ya chumvi au baharini.
Huchimbwa hasa Australia, Skandinavia, Amerika ya Kaskazini, Malaysia na Afrika Kusini.
Barani Afrika imeanza kuchimbwa pia Kenya, Msumbiji na Sierra Leone. Katika nchi hizo makampuni yanayoichimba pamoja na serikali zimepingwa mara nyingi kwa sababu ya hatari kwa ajili ya mazingira kutokana na uchimbaji na usimamizi hafifu.