Tovuti (Kiing. website)[1] ni mkusanyiko wa kurasa zilizoandikwa kwa lugha mbalimbali za tarakilishi kama vile HTML, PHP, XHTML na kadhalika na ambazo kwa pamoja hujumuika katika kutoa habari au maelezo kuhusu jambo fulani. Lugha hizi, yaani HTML, PHP, XHTML na kadhalika zinaweza tu kusomwa na kutafsiriwa na programu kama vile Internet Explorer Google Chrome na Mozilla Firefox kwa lugha ambayo inaweza kueleweka na binadamu. Wingi wake ni "tovuti" vile vile. Tovuti zote pamoja zinaitwa "mtandao" au "Intaneti" au "wavuti".