Tragelaphus

Kwa matumizi tofauti ya jina hili angalia hapa Tandala (Makete)

Tandala
Dume la tandala mkubwa (Tragelaphus strepsiceros)
Dume la tandala mkubwa
(Tragelaphus strepsiceros)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyana wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Artiodactyla (Wanyama wenye vidole viwili au vinne mguuni)
Nusuoda: Ruminantia (Wanyama wanaocheua)
Familia: Bovidae (Wanyama walio na mnasaba na ng'ombe)
J. E. Gray, 1821
Jenasi: Tragelaphus (Nyala, pongo na tandala)
de Blainville, 1816
Ngazi za chini

Spishi 8:

Tragelaphus ni jenasi ya wanyama katika familia Bovidae. Spishi za Tragelaphus huitwa tandala, bongo, kulungu, malu, nyala au nzohe.

Wanatokea Afrika katika maeneo yenye miti kutoka nyika hadi msitu.

Wana milia na madoa meupe juu ya rangi ya kahawa au kijivu. Dume ni mkubwa kuliko jike na ana pembe ndefu zilizopotolewa. Jike hana pembe.

Wanyama hao hula majani, manyasi, matunda na viazi vya gugu.


Tragelaphus

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne