Uhalisia (kutoka Kiarabu "halisi"; kwa Kiingereza Reality) ni hali iliyopo kweli, tofauti na matarajio au tafsiri za binadamu ambaye mara nyingi anashindwa kuipokea.[1]
Kwa upana zaidi, uhalisia unajumlisha hata mambo yasiyofikiwa na milango ya fahamu, vifaa na mawazo ya binadamu.
Wanafalsafa, wanahisabati, wanasayansi na wengineo wamejitahidi tangu zamani kuelewa uhalisia, wakitoa majibu mbalimbali.
Mara nyingi uhalisia unagonganishwa na ndoto na ndoto za mchana, maigizo na propaganda, pamoja na uongo wa kila namna.