Uhodhisoko (kutokana na kitenzi "kuhodhi" na neno "soko"; kwa Kiingereza "monopoly", kutoka maneno mawili ya Kigiriki: monos, yaani "pekee", na polein, yaani "kuuza") ni hali ya uchumi ambapo watu wachache au kampuni chache, kama si moja tu, hudhibiti soko la bidhaa fulani kiasi kwamba washindani hawawezi kuliingilia. Hali hiyo inaathiri upangaji wa bei na mambo mengine yanayohusu bidhaa hiyo.