Ujauzito ni hali ya mja (yaani mtu, hususan mwanamke) kuwa mzito kutokana na mimba.
Hali hiyo kwa kawaida inadumu wiki 38 (miezi tisa hivi) ambapo mimba inazidi kukua na kukomaa ndani ya tumbo la uzazi la mama yake hadi wakati wa huyo kujifungua.
Ingawa katka lugha kadhaa yanatumika majina mbalimbali kwa mimba hiyohiyo kadiri muda wa kukua unavyozidi kwenda, hakuna badiliko la msingi wala hatua mpya, bali ni ustawi endelevu.
Miezi mitatu ya kwanza ndiyo yenye hatari zaidi ya mimba kuharibika.
Pengine mimba si moja bali mbili au zaidi kwa wakati mmoja. Hapo watazaliwa watoto pacha.