Utani ni maneno ya mzaha yenye ukweli ndani yake. Utani kama kipengele kimojawapo cha sanaa na maigizo huonesha uhusiano mwema wa jamii unaowawezesha wanajamii hao kufanyiana maneno ya mzaha na hata kuchukuliana vitu bila kukasirikiana.
Utani unaweza kuwa kati ya mtu na mtu, ukoo na ukoo au kabila na kabila. Katika nchi ya Tanzania umechangia sana kumaliza au kuepusha vita na shari nyingi baada ya makabila adui kuamua kutambuana kama watani, k.mf. Wangoni na Wahehe.