Vichekesho ni maigizo mafupi yenye lengo la kufikisha ujumbe kwa njia ya kufurahisha au kuchekesha hadhira husika. Vichekesho huundwa kwa mpangilio wa maneno ulio na utendekaji ambao hauna kina kuhusu kisa kinachooneshwa - huonesha kisa au jambo bila kulichambua kwa kina.
Vichekesho hutumia wahusika ambao hutumia lugha nyepesi ya picha na tamathali ambazo watazamaji wana uwezo wa kuzitambua. Vichekesho huigizwa kwenye runinga, redioni, shuleni, na kwenye sherehe mbalimbali.